Mbinu za Shetani.





Jina la Yesu lisifiwe!!
Karibu ndugu yangu tujifunze juu ya mbinu na mikakati ya shetani dhidi ya wote wamwaminio yesu kristo. Tunapompokea Yesu tunatangaza vita na shetani. Ibilisi hutumia mbinu zote ili kuhakikisha mteule wa kristo anarudi nyma na kumwacha Bwana Yesu.
Neno la Mungu linasema,” Mwe na kiasi na kukesha, kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, ni kama Simba aungurumaye, huzunguka – zunguka akitafuta mtu ammeze” 1 Petro 5:8
Ibilisi ni mshitaki /adui yetu, huzunguka huku na kule akitafuta mtu amwangamize, yaani wale wamwaminio kristo. Pia Neno la Mungu linasema,” Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za shatani kwa maana kushindana kwetu si juu yadamu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya….” – Efeso 6:11,12.
        Tupo vitani ulimwenguni, yeyote amwaminiye Yesu kristo yupo vitani dhidi ya Ufalme wa shetani na majeshi yake, amejipanga kuhakikisha wakristo hawafanikiwi kumpendeza Mungu wao. Nia yake kuu ni kutuzuia tusiishi maisha safi (matakatifu) na tusimtumikie Yesu kristo na mwisho tuukose uzima wa milele mbinguni.
Bibilia inasema, tuvae silaha zote za Mungu. Pia tukeshe na kuwa na kiasi, tudumu katika Neno la Mungu na maombi siku zote. Pia tuwe na upendo kwani huo ndio ukamilifu wa mambo yote (Rum 13:10)
Zifuatazo ni baadhi ya mbinu mahususi za Ibilisi dhidi ya wateule wa Yesu kristo. Hii ni Barua elekezi ya shetani (Lucifer) kwa mawakala (watumishi) wake, jinsi ya ya kupambana na wateule wa Mungu ili kuwashinda. Ingawa ni mambo ya siri lakini Mungu ameyaleta nuruni ili tupate ufahamu. Soma kwa moyo uliofunguka.

       INASIKITISHA SANA!!! Lucifer, mkuu wa mashetani (ufalme wa giza) aliitisha semina elekezi kwa mashetani wote duniani (wachawi, mapepo, majini, n.k) na katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo alisema:-
“ Tumeshinda kuwazuia wakristo wasiende kanisani. Tumeshindwa kuwazuia wakristo wasisome Biblia zao kufahamu ukweli ( shetani anajua kuwa Neno la mungu limebeba ukweli ndani yake). Pia tumeshindwa hata kuwazuia wasiwe na mapenzi ya kweli ( upendo halisi) kwa mwokozi wao ( Yesu kristo). Mara wapatapo muungano wa kweli  (ukaribu mkubwa na halisi) na Kristo, mamlaka yetu yatakuwa yamefikia mwisho” – ( Ibilisi anajua kuwa ukaribu wetu kwa Yesu ndiko kushindwa kwake, naye atatumia mbinu zote kuzuia hilo). LUCIFER akasema;-
“ kwa hiyo waacheni waende kanisani, waacheni waendelee na karamu zao za upendo, lakini waibieni MUDA, ili wasipate nafasi ya kudumisha mahusiano (ukaribu)  na mapenzi ya kweli kwa Yesu kristo “ Hiki ndicho ninachotaka mfanye’ alisema Lucifer,” wataabisheni ili ili wasipate kamwe nafasi ya kushikamanana mwokozi wao, wasifungamane naye kwa siku nzima” (wakose muda wa kumtafakari Yesu kristo, kusoma Biblia na kuomba).
Tutafanyje mambo hayo, mashetani yalimwuliza kwa jazba. Lucifer akasema, “hakikisheni wanakuwa busy, (BUSY= Being under satans York) katika mambo yasiyokuwa na umuhimu katika maisha yao. Pia wafanyeni wawe na mipango mingi sana isiyohesabika ili kujuza akili zao na ufahamu wao ( hivyo kuwa busy kila wakati, hata ibada usiende ). Aliendelea kusema wafanyeni kutumiafedha, na kutumia na kutumia na kukopa na kukopa”
Washawishini wake zao waende kufanya kazi kwa siku nzima na kushinda huko, na waume zao wafanye kazi siku sita hadi saba kwa wiki, na masaa 10 hadi 12 kwa siku. Kwa njia hiyo watashindwa kutulia na kutafakari chochote kulingana na mfumo huo wa maisha. Watakosa muda wa kumwabudu  na kumtafuta mwoko
“Wazuieni wazazi wasiwe na nafasi ya kukaa na watoto wao, Familia zao zikivurugika, mara nyumba zao hazitakwepa msongamano wa kazi na mawazo”
“hakikisheni mnachochea na kusumbua zaidi akili na fahamu zao ili kuhakikisha hawaisikii ile sauti ndogo, tulivu ya Mungu wao” – sauti ya Roho mt.
Washawishini walize redio au kaseti au mziki kwenye simu, popote wanapoendesha gari au wanapotembea kwa miguu. Waziache TV, VCR, CD na Komputa zikiwa zikiwa zimewashwa muda wote, pia mhakikishe kila duka na mgahawa kote duniani linapiga muziki usio wa kibibilia mfululizo bila kikomo. Njia hii itasonga akili na fahamu zao na kuweza kuvunja ule muungano ( ukaribu) wao na Yesu wao.
Pia, jazeni magazeti na vijarida kwenye meza za kahawa na chai duniani kote. Shindilieni habari na matukio mbalimbali ndani ya fahamu zao kwa masaa 24. Ingilieni muda wao na kuendesha barabarani kwa kuwaonyesha mabango na matangazo. Kwenye masanduku ya posta na barua pepejazeni vipeperushi na majarida na kila aina ya matangazo ya habari za vitu na huduma, yanayowapa matumaini ya uongo, Hii itazuia wasimtafakari mwokozi wao wala Neno lake, na hivyo watapungukiwa nguvu za Yesu.
Lucifer aliendelea kusema, “wekeni wanawake warembo sana mitaani, club; maofisini na
kwenye televisheni na majarida. Hii itawafanya wanaume walioko kwenye ndoa wadanganyike na kuamini kwamba urembo wanje ndio muhimu na wasiridhike na wake zao... Wafanyeni wake zao wachoke sana hata kushindwa kuonyesha upendo kwa waume zao usiku. Kama hawatawapa waume zao upendo wanaohitajika sana, waume zao wataanza kutazama na kutamani kwingine. Njia hiyo itavuruga ndoa na familia zao haraka sana. Pia pelekeni walimu wa uongo ili wawapotoshe wakristo, wasifundishe injili ya kweli kwa watoto wao na waumini wao.
Lucifer aliendelea, “ majira ya kukumbuka kufa na kufufuka kwa Yesu wao, wapeni zawadi na kadi za pasaka ili wasahau kuzungumzia juu ya nguvu za kufufuka kwa Yesu wao dhidi ya dhambi na mauti.Hii itawafanya wasahau kazi aliyoifanya Yesu wao msalabani. Fanyeni hili pia nyakati za wao kukumbuka kuzaliwa kwa kristo Hata katika karamu zao wachosheni sana  kwa anasa na kuwafanya warudi wamechoka sana.
 Hakikisheni wanakuwa “BUSY” yaani wasongwe sana na mambo/kazi kiasi kwamba hawapati nafasi ya kutafakari wema wa Mungu na kudumisha uhusiano na Yesu wao. Nyakati za mapumziko na likizo, wapeni kutalii kwenye maeneo ya ajabu, matukio ya michezo, kwenye maeneo ya ajabu, matukio ya michezo, matamasha na kumbi za sinema na video. Wafanyeni wawe “BUSY, BUSY, BUSY; yaani wasongwe na kusongwa na kazi kwelikweli. Namna hii watakosa nafasi ya kudumisha uhusiano wao na kristo, hata muda wa Ibada wawe BUSY. (mfano kutumia simu muda na kutafakari mambo mengine muda wa ibada)
“Na wanapokutanika ibada zao za kiroho, wafanyeni waingie katika umbea na fitina na kuzungumzia mambo madogo madogo ya umbea na fitina ili waondoke ibadani wakiwa na dhamira mbaya zilizochafuliwa” alisema Lucifer.
“Jazeni visababishi vingi vya mambo katika maisha yao ili wakose nafasi na muda wa kutafuta msaada na nguvu za Yesu” – ( kusoma Neno, kuomba, kwenda Ibadani). Kwa njia hizo, muda si mrefu, bila wao kujua, muunganiko (ukaribu) wao na Kristo utavunjika,  na ndipo tutafanikiwa kuwashinda... Mwisho wa ujumbe wa Lucifer.
Ndugu yangu huu ni wakati wa kuamka na kumtumikia Yesu kwa bidii. Ni saa ya kudumu katika neno la Mungu na  kulitii, na kudumu katika maombi . Shetani anaogopa sana, pale wateule wanapokuwa na muunganiko (uhusiano wa ukaribu) wa kweli na Yesu , kwani mamlaka yake hufika mwisho.
Ndugu tatafute kuwa karibu na Bwana zaidi, tafuta kumpendeza yeye, mtii yeye kila wakati. Tukatae kubanwa na mambo / kazi kiasi cha kukosa nafasi ya kudumisha uhusiano na Bwana wetu kukosa kwenda ibada, kusoma Neno, kuomba. Mpe Mungu nafasi ya kwanza ktk maisha yakona mambo mengine yafuate. Mbingu zimeandaliwa kwa ajili yetu tumwaminio Yesu, hivyo tukaze mwendo, na kujitoa kwa Mungu.
Endelea kumtafuta Mungu na kutafuta kuzijua mbinu za adui  yetu. Unaweza kutuma ujumbe huu kwa ndugu, jamaa na marafiki.
Mungu wa mbinguni akubariki sana.

Comments

Popular posts from this blog

SISI NI WAPITAJI DUNIANI