SISI NI WAPITAJI DUNIANI
SISI NI WAPITAJI DUNIANI Shukrani kwa Mungu kwa nafasi hii ya kutafakari habari njema. Kama kichwa kinavyosema, wanadamu wote ni wapitaji ulimwenguni. Hatujapewa makao ya milele hapa Duniani, lakini baada ya maisha ha ya kuna makao ya milele kwa kila mwanadamu. Mtume Paulo anasema katika waebrania 13:14, “ Maana hapa hatuna mji (makao) udumuo, bali twautafuta ule ujao” . Ni mji upi huo anasema wanautafuta au wanatamani kuufikia. Ni mji au makao ya mbinguni, Ndivyo Yesu kristo alivyosema, “ maana naenda kuwaandalia mahali (makao). Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja (nitarudi) tena niwakaribishe kwangu ili nilipo mimi, nanyi mwepo” Yohana 14:2. Yesu aliwaeleza wanafunzi wake juu ya makao ambayo anakwenda kuwaandalia mbinguni. Biblia inaeleza wazi kuhusu maisha ya milele ya mwanadamu baada ya Dunia hii. Kuna...