Posts

SISI NI WAPITAJI DUNIANI

SISI NI WAPITAJI      DUNIANI Shukrani kwa Mungu kwa nafasi hii ya kutafakari habari njema.     Kama kichwa kinavyosema, wanadamu   wote ni wapitaji ulimwenguni. Hatujapewa makao ya milele hapa Duniani, lakini baada ya maisha ha ya kuna makao ya milele kwa kila mwanadamu. Mtume Paulo anasema katika waebrania 13:14, “ Maana hapa hatuna mji (makao) udumuo, bali twautafuta ule ujao” . Ni mji upi huo anasema wanautafuta   au wanatamani kuufikia. Ni mji au makao ya mbinguni, Ndivyo Yesu kristo alivyosema, “ maana naenda kuwaandalia mahali (makao). Basi mimi   nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja (nitarudi) tena niwakaribishe kwangu ili nilipo mimi, nanyi mwepo” Yohana 14:2. Yesu aliwaeleza wanafunzi wake juu ya makao ambayo anakwenda kuwaandalia mbinguni.                 Biblia inaeleza wazi kuhusu maisha ya milele ya mwanadamu baada ya Dunia hii. Kuna...

Mbinu za Shetani.

                             MBINU NA MIKAKATI YA SHETANI DHIDI YAKO. Jina la Yesu lisifiwe!! Karibu ndugu yangu tujifunze juu ya mbinu na mikakati ya shetani dhidi ya wote wamwaminio yesu kristo. Tunapompokea Yesu tunatangaza vita na shetani. Ibilisi hutumia mbinu zote ili kuhakikisha mteule wa kristo anarudi nyma na kumwacha Bwana Yesu. Neno la Mungu linasema ,” Mwe na kiasi na kukesha, kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, ni kama Simba aungurumaye, huzunguka – zunguka akitafuta mtu ammeze” 1 Petro 5:8 Ibilisi ni mshitaki /adui yetu, huzunguka huku na kule akitafuta mtu amwangamize, yaani wale wamwaminio kristo. Pia Neno la Mungu linasema,” Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za shatani kwa maana kushindana kwetu si juu yadamu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya p...